Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Msemaji wa Jeshi la Yemen, Yahya Saree amesema: Tumelenga na kuutwanga Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion ulioko katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Yafa kwa kombora la Balistiki lenye kasi ya juu aina ya Palestine-2.
Operesheni za Yemen zitaendelea hadi vita na mzingiro dhidi ya Gaza utakapositishwa.
Aisha, Wananchi wa Yemen wameendelea kuonyesha sapoti yao kubwa kwa Wananchi wa Palestina hususan Ghaza kwa kujitokeza katika Maandamano ya kukemea Mauaji ya Utawala haram wa Kizayuni dhidi ya Wanawake na Watoto katika ukanda wa Ghaza na kuitaka Israel ikomeshe mara moja mzingiro wake dhidi ya Ghaza na Mauaji yake ya halaiki dhidi Wananchi wa ukanda huo wa Ghaza.
Your Comment